6 Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Maandiko yasema:
"Mungu huwapinga wenye kiburi,
lakini huwapa wanyenyekevu neema."
7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. 8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. 9 Huzunikeni, na mwomboleze, na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni. 10 Jinyenyekezeni mbele za Mwenyezi Mungu, naye atawainua.