Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Wakorintho 12:4-7,12,27

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

4 Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. 5 Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana Isa ni yule yule. 6 Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.

7 Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho wa Mungu kwa faida ya wote.

Mwili mmoja wenye viungo vingi

12 Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi; navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Al-Masihi.

27 Sasa ninyi ni mwili wa Al-Masihi na kila mmoja wenu ni sehemu ya huo mwili.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    4 Rum 12:6-8;Efe 4:4Basi kuna karama tofauti; bali Roho ni yeye yule. 5 Efe 4:11Tena kuna huduma tofauti, na Bwana ni yeye yule. 6 Kisha kuna uwezo tofauti wa kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. 7 1 Kor 14:26Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.

    12 Rum 12:4-5;1 Kor 10:17Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. 27 Rum 12:5;Efe 5:30Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na kila mmoja wenu akiwa kiungo cha mwili huo.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    4 Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. 5 Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule. 6 Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.

    7 Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote.

    12 Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi, navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo.

    27 Sasa ninyi ni mwili wa Kristo na kila mmoja wenu ni sehemu ya huo mwili.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.