3 Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Al-Masihi alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama Maandiko yanavyosema, 4 ya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama Maandiko yanavyosema, 5 na kwamba alimtokea Kefa15:5 yaani Petro, kisha akawatokea wale kumi na wawili. 6 Baadaye akawatokea wale ndugu waumini zaidi ya mia tano kwa pamoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengine wamelala.
Publicidade