3 Huku ndiko kumpenda Mungu, yaani kuzitii amri zake. Nazo amri zake si nzito. 4 Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani hiyo imani yetu. 5 Ni nani yule aushindaye ulimwengu? Ni yule tu aaminiye kwamba Isa ni Mwana wa Mungu5:5 Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (Yohana 1:1-2), wa kiroho, bali si wa kimwili..
Publicidade