23 Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu inayoharibika, bali kwa mbegu isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu milele. 24 Maana,
"Wanadamu wote ni kama majani,
nao utukufu wao wote ni kama maua ya kondeni;
majani hunyauka na maua huanguka,
25 lakini neno la Mwenyezi Mungu ladumu milele."
Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.