Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samweli 19

11 Sauli akatuma watu nyumbani mwa Daudi wailinde hiyo nyumba na kumuua asubuhi. Lakini Mikali, mkewe Daudi, akamwonya akisema, "Usipokimbia kuokoa maisha yako usiku huu, kesho utauawa." 12 Basi Mikali akamteremsha Daudi kupitia dirishani, naye akakimbia na kuokoka. 13 Kisha Mikali akachukua kinyago, akakilaza kitandani, akakifunika kwa vazi na kukiwekea singa za mbuzi kichwani.

14 Sauli alipotuma watu kumkamata Daudi, Mikali akasema, "Yeye ni mgonjwa."

15 Kisha Sauli akatuma watu tena kumwona Daudi naye akawaambia, "Mleteni kwangu juu ya kitanda chake ili nipate kumuua." 16 Lakini wale watu walipoingia, kumbe ni kinyago tu kilichokuwa kitandani, na kwenye kichwa kulikuwa na singa za mbuzi.

17 Sauli akamwambia Mikali, "Kwa nini umenidanganya mimi hivi na kumwacha adui yangu aende zake ili apate kuokoka?"

Mikali akamwambia, "Yeye aliniambia, Niache niende zangu. Kwa nini nikuue?’ "

18 Daudi alipokuwa amekimbia na kuokoka, alimwendea Samweli huko Rama na kumwambia yale yote Sauli alimfanyia. Ndipo Daudi na Samweli wakaenda Nayothi kukaa huko.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também