Maombi ya Hana
1 Kisha Hana akaomba na kusema:
"Moyo wangu wamshangilia Mwenyezi Mungu,
katika Mwenyezi Mungu pembe2:1 pembe inawakilisha nguvu yangu imeinuliwa juu.
Kinywa changu chajisifu juu ya adui zangu,
kwa kuwa naufurahia wokovu wako.
2 "Hakuna yeyote aliye mtakatifu kama Mwenyezi Mungu,
hakuna mwingine zaidi yako;
hakuna Mwamba kama Mungu wetu.
3 "Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo
wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi,
kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu ajuaye,
na yeye hupima matendo.
4 "Pinde za mashujaa zimevunjika,
lakini wale wanaojikwaa wamevikwa nguvu.
5 Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe
ili kupata chakula,
lakini wale waliokuwa na njaa
hawana njaa tena.
Mwanamke yule aliyekuwa tasa
amezaa watoto saba,
lakini yule aliyekuwa na wana wengi
amedhoofika.
6 "Mwenyezi Mungu huua na huhuisha;
yeye hushusha hadi kaburini2:6 Kaburini maana yake ni Kuzimu; kwa Kiebrania ni Sheol. na hufufua.
7 Mwenyezi Mungu humfanya mtu maskini naye hutajirisha,
hushusha na hukweza.
8 Humwinua maskini kutoka mavumbini
na humwinua mhitaji kutoka lundo la majivu;
huwaketisha pamoja na wakuu,
na kuwafanya warithi kiti cha utawala cha heshima.
"Kwa kuwa misingi ya dunia ni ya Mwenyezi Mungu;
juu yake ameuweka ulimwengu.
9 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake,
lakini waovu watanyamazishwa kwenye giza.
"Si kwa nguvu mtu hushinda;
10 wale wampingao Mwenyezi Mungu
wataharibiwa kabisa.
Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni;
Mwenyezi Mungu ataihukumu miisho ya dunia.
"Atampa nguvu mfalme wake,
na kuitukuza pembe
ya mpakwa mafuta wake."