Kitabu na Mwana-Kondoo
1 Kisha nikaona katika mkono wake wa kuume wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, kitabu kilichoandikwa ndani na nje, kikiwa kimefungwa kwa mihuri saba. 2 Nami nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, "Ni nani anayestahili kuivunja hiyo mihuri na kukifungua kitabu?"