18"Kisha atatoka aje kwenye madhabahu yaliyo mbele za Mwenyezi Mungu na kufanya upatanisho kwa ajili yake. Atachukua sehemu ya damu ya fahali na sehemu ya damu ya mbuzi, na kuiweka kwenye pembe za madhabahu.
31Ni Sabato ya mapumziko, na lazima mfunge; ni agizo la kudumu.
33na kufanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu, Hema la Kukutania na madhabahu, na pia kwa ajili ya makuhani, pamoja na jumuiya yote ya watu.