Baraka za utiifu
1 Ukimtii Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa ukamilifu na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa makini, Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia. 2 Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtii Mwenyezi Mungu, Mungu wako:
12 Mwenyezi Mungu atafungua mbingu, ghala zake za baraka, kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mikono yako. Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa yeyote.