Baraka za utiifu
1 Kum 11:13-17;Kut 15:26;Law 26:3;Zab 106:3;111:10;Isa 1:19;3:10;Yer 11:4;12:16;1 Nya 14:2;Rum 2:10Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 2 Zek 1:6na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. 12 Yak 1:18Atakufunulia BWANA hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.