Pular para o conteúdo
Publicidade

Kumbukumbu La Torati 3:23-28

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

23 Wakati huo nilimsihi Mwenyezi Mungu: 24 "Ee Bwana Mungu Mwenyezi, umemwonesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliye mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe? 25 Acha niende nikaione hiyo nchi nzuri ng’ambo ya Yordani, ile nchi nzuri ya vilima na Lebanoni."

26 Lakini kwa sababu yenu Mwenyezi Mungu alinikasirikia na hakutaka kunisikiliza. Mwenyezi Mungu aliniambia, "Hilo latosha; usiseme nami jambo hili tena. 27 Kwea juu ya kilele cha Pisga uangalie magharibi, kaskazini, kusini na mashariki. Iangalie hiyo nchi kwa macho yako, kwa vile wewe hutavuka Yordani. 28 Lakini mwagize Yoshua, mtie moyo na umtie nguvu, kwa kuwa yeye atawaongoza watu hawa hadi ng’ambo na kuwarithisha nchi utakayoiona."

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    23 Hes 27:12-14;Kum 32:48-52Nikamnyenyekea BWANA wakati huo, nikamwambia, 24 Kum 11:2;Neh 9:32;Zab 106:2;145:3,6;Yer 32:18-21;Kut 15:11;2 Sam 7:22;Zab 71:19;86:8Ee BWANA Mungu, umeanza kumwonesha mtumishi wako ukubwa wako, na mkono wako wa nguvu; kwani kuna mungu gani mbinguni au duniani awezaye kufanya mfano wa kazi zako, na mfano wa matendo yako yenye nguvu? 25 Kut 3:8;Kum 4:22Nami nakuomba nivuke, nikaione hiyo nchi nzuri iliyoko ng’ambo ya Yordani, mlima ule mzuri, na Lebanoni. 26 Lakini BWANA alikuwa amenikasirikia kwa ajili yenu, asinisikize; BWANA akaniambia, Na ikutoshe, usinene nami zaidi jambo hili. 27 Kwea katika kilele cha Pisga ukainue macho yako upande wa magharibi, na kaskazini, na kusini, na mashariki, ukatazame kwa macho yako, kwa maana huuvuki mto huu wa Yordani. 28 Hes 27:18;Kum 1:38;31:3,7Lakini mwagize Yoshua, mtie moyo na nguvu, umtie na nguvu; kwani ndiye atakayevuka mbele ya watu hawa, na nchi utakayoiona atawarithisha yeye.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    23 Wakati huo nilimsihi Bwana: 24 "Ee Bwana Mwenyezi, umemwonyesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliye mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe? 25 Acha niende nikaione hiyo nchi nzuri ngʼambo ya Yordani, ile nchi nzuri ya vilima na Lebanoni."

    26 Lakini kwa sababu yenu Bwana alinikasirikia na hakutaka kunisikiliza. Bwana aliniambia, "Hilo latosha; usiseme nami jambo hili tena. 27 Kwea juu ya kilele cha Pisga uangalie magharibi, kaskazini, kusini na mashariki. Iangalie hiyo nchi kwa macho yako, kwa vile wewe hutavuka Yordani. 28 Lakini mwagize Yoshua, mtie moyo na umtie nguvu, kwa kuwa yeye atawaongoza watu hawa hadi ngʼambo na kuwarithisha nchi utakayoiona."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.