Musa aitazama Kanaani kutoka Pisga
23 Hes 27:12-14;Kum 32:48-52Nikamnyenyekea BWANA wakati huo, nikamwambia, 24 Kum 11:2;Neh 9:32;Zab 106:2;145:3,6;Yer 32:18-21;Kut 15:11;2 Sam 7:22;Zab 71:19;86:8Ee BWANA Mungu, umeanza kumwonesha mtumishi wako ukubwa wako, na mkono wako wa nguvu; kwani kuna mungu gani mbinguni au duniani awezaye kufanya mfano wa kazi zako, na mfano wa matendo yako yenye nguvu? 25 Kut 3:8;Kum 4:22Nami nakuomba nivuke, nikaione hiyo nchi nzuri iliyoko ng’ambo ya Yordani, mlima ule mzuri, na Lebanoni. 26 Lakini BWANA alikuwa amenikasirikia kwa ajili yenu, asinisikize; BWANA akaniambia, Na ikutoshe, usinene nami zaidi jambo hili. 27 Kwea katika kilele cha Pisga ukainue macho yako upande wa magharibi, na kaskazini, na kusini, na mashariki, ukatazame kwa macho yako, kwa maana huuvuki mto huu wa Yordani. 28 Hes 27:18;Kum 1:38;31:3,7Lakini mwagize Yoshua, mtie moyo na nguvu, umtie na nguvu; kwani ndiye atakayevuka mbele ya watu hawa, na nchi utakayoiona atawarithisha yeye.