4 Sikia, ee Israeli: Mwenyezi Mungu, Mungu wako, Mwenyezi Mungu ni mmoja. 5 Mpende Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. 7 Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.
20 Siku zijazo, mtoto wako atakapokuuliza, "Ni nini maana ya masharti haya, amri na sheria hizi ambazo Mwenyezi Mungu, Mungu wako, alikuagiza wewe?" 21 Mwambie: "Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, lakini Mwenyezi Mungu alitutoa sisi kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu.