Pular para o conteúdo
Publicidade

Kumbukumbu la Torati 6:4-7,20,21

SRUV Swahili Revised Union Version

4 Mk 12:29;Isa 9:6;Yn 1:1;10:30;17:3;1 Kor 8:4;Efe 4:6;Flp 2:5,6Sikiliza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja6:4 Au Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; au Bwana Mungu wetu ni mmoja; au Bwana ni Mungu wetu, Bwana ni mmoja.5 Mt 22:37;Mk 12:30-32;Lk 10:27;Kum 30:6;1 Yoh 5:3Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 Kum 11:18-20;Isa 51:7Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; 7 Efe 6:4nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

20 Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, Ni nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu? 21 Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu;

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    4 Sikia, ee Israeli: Mwenyezi Mungu, Mungu wako, Mwenyezi Mungu ni mmoja. 5 Mpende Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. 7 Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.

    20 Siku zijazo, mtoto wako atakapokuuliza, "Ni nini maana ya masharti haya, amri na sheria hizi ambazo Mwenyezi Mungu, Mungu wako, alikuagiza wewe?" 21 Mwambie: "Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, lakini Mwenyezi Mungu alitutoa sisi kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    4 Sikia, ee Israeli: Bwana Mungu wako, Bwana ni mmoja. 5 Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. 7 Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.

    20 Siku zijazo, mtoto wako atakapokuuliza, "Ni nini maana ya masharti haya, amri na sheria hizi ambazo Bwana Mungu wako alikuagiza wewe?" 21 Mwambie: "Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, lakini Bwana alitutoa sisi kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.