18 Ndipo tena nikasujudu hadi chini mbele za Mwenyezi Mungu kwa siku arobaini usiku na mchana. Sikula mkate wala sikunywa maji, kwa sababu ya dhambi yote mliyoifanya, mkifanya lile lililo ovu mbele za Mwenyezi Mungu na kumkasirisha. 19 Niliogopa hasira na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa aliwakasirikia ninyi sana na kutaka kuwaangamiza. Bali Mwenyezi Mungu alinisikiliza tena.
25 Nilianguka kifudifudi mbele za Mwenyezi Mungu kwa zile siku arobaini usiku na mchana kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuwa amesema angewaangamiza ninyi. 26 Nilimwomba Mwenyezi Mungu na kusema, "Ee Bwana Mungu Mwenyezi, usiangamize watu wako, urithi wako mwenyewe ule ulioukomboa kwa uweza wako mkuu na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu.