Pular para o conteúdo
Publicidade

Kumbukumbu la Torati 9:18,19,25,26

SRUV Swahili Revised Union Version

18 Kut 34:28;Zab 106:23Nikaanguka chini mbele za BWANA siku arubaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyofanya, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kwa kumkasirisha. 19 Ebr 12:21,29;Kut 32:10,11,14;33:17;Kum 10:10;Zab 106:23;Yak 5:15;Amo 7:1-6Kwa kuwa niliogopa hasira na makamio aliyowakasirikia BWANA kutaka kuwaangamiza. Lakini BWANA alinisikiza wakati huo nao. 25 Ndipo nikaanguka chini mbele za BWANA siku zile arubaini usiku na mchana nilizokuwa nimeanguka chini; kwa kuwa BWANA alisema atawaangamiza. 26 Kut 32:11;1 Sam 7:9;Mit 15:29;Yer 15:1Nikamwomba BWANA, nikasema, Ee Bwana Mungu, usiwaangamize watu wako, urithi wako, uliowakomboa kwa ukuu wako, uliowatoa Misri kwa mkono wa nguvu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    18 Ndipo tena nikasujudu hadi chini mbele za Mwenyezi Mungu kwa siku arobaini usiku na mchana. Sikula mkate wala sikunywa maji, kwa sababu ya dhambi yote mliyoifanya, mkifanya lile lililo ovu mbele za Mwenyezi Mungu na kumkasirisha. 19 Niliogopa hasira na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa aliwakasirikia ninyi sana na kutaka kuwaangamiza. Bali Mwenyezi Mungu alinisikiliza tena.

    25 Nilianguka kifudifudi mbele za Mwenyezi Mungu kwa zile siku arobaini usiku na mchana kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuwa amesema angewaangamiza ninyi. 26 Nilimwomba Mwenyezi Mungu na kusema, "Ee Bwana Mungu Mwenyezi, usiangamize watu wako, urithi wako mwenyewe ule ulioukomboa kwa uweza wako mkuu na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    18 Ndipo tena nikasujudu mbele za Bwana kwa siku arobaini usiku na mchana. Sikula mkate wala sikunywa maji, kwa sababu ya dhambi yote mliyoifanya, mkifanya lile lililo ovu mbele za Bwana na kumkasirisha. 19 Niliogopa hasira na ghadhabu ya Bwana, kwa kuwa aliwakasirikia vya kutosha na kutaka kuwaangamiza. Lakini Bwana alinisikiliza tena.

    25 Nilianguka kifudifudi mbele za Bwana kwa zile siku arobaini usiku na mchana kwa sababu Bwana alikuwa amesema angewaangamiza ninyi. 26 Nilimwomba Bwana na kusema, "Ee Bwana Mwenyezi, usiangamize watu wako, urithi wako mwenyewe ule ulioukomboa kwa uweza wako mkuu na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.