Pular para o conteúdo
Publicidade

Mhubiri 4:6-8

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

6 Afadhali konzi moja pamoja

na utulivu kuliko konzi mbili pamoja na taabu

na kukimbiza upepo.

7 Tena nikaona kitu kingine kilicho ubatili chini ya jua:

8 Kulikuwa na mtu aliye peke yake,

hakuwa na mwana wala ndugu.

Hapakuwa na mwisho wa kazi yake;

hata hivyo macho yake

hayakutosheka na utajiri wake.

Aliuliza, "Ninajitaabisha hivi kwa ajili ya nani,

nami kwa nini ninajinyima kufurahia?"

Hili pia ni ubatili,

ni shughuli yenye taabu!

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    6 Heri konzi moja pamoja na utulivu,

    Kuliko konzi mbili pamoja na taabu;

    na kufukuza upepo.

    7 Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua. 8 Mit 27:20;Mhu 1:8;Hab 2:5,6;1 Yoh 2:16;Zab 39:6;Lk 12:20Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    6 Afadhali konzi moja pamoja

    na utulivu kuliko konzi mbili pamoja na taabu

    na kukimbiza upepo.

    7 Tena nikaona kitu kingine kilicho ubatili chini ya jua:

    8 Kulikuwepo mwanadamu aliye peke yake,

    hakuwa na mwana wala ndugu.

    Hapakuwa na mwisho wa kazi yake,

    hata hivyo macho yake

    hayakutosheka na utajiri wake.

    Aliuliza, "Ninajitaabisha hivi kwa ajili ya nani,

    nami kwa nini ninajinyima kufurahia?"

    Hili pia ni ubatili,

    ni shughuli yenye taabu!

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.