20 Kisha Miriamu yule nabii mke, ndugu yake Haruni, akachukua matari mkononi mwake na wanawake wote wakamfuata na matari yao wakicheza. 21 Miriamu akawaimbia:
"Mwimbieni Mwenyezi Mungu,
kwa maana ametukuka sana.
Farasi na mpanda farasi
amewatosa baharini."