Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 2

Kuzaliwa kwa Musa

1 Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi, 2 naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu. 3 Lakini alipoona hawezi kuendelea kumficha, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha kwenye matete kando ya ukingo wa Mto Naili. 4 Dada ya huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto.

5 Ndipo binti Farao akateremka kwenye Mto Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti Farao akaona kisafina kwenye matete, akamtuma mmoja wa wajakazi wake kukichukua. 6 Alifungua kisafina akaona mtoto ndani yake. Mtoto alikuwa akilia, akamhurumia. Akasema, "Huyu ni mmoja wa watoto wa Waebrania."

7 Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, "Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Waebrania akulelee huyu mtoto?"

8 Binti Farao akamjibu, "Ndiyo, nenda." Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto. 9 Binti Farao akamwambia, "Mchukue huyu mtoto unisaidie kumlea, nami nitakulipa." Basi yule mwanamke akamchukua mtoto na kumlea. 10 Mtoto alipokua, akampeleka kwa binti Farao, naye akawa mwanawe. Akamwita jina Musa, akisema, "Nilimtoa kwenye maji."

Veja também