14 Mungu akamwambia Musa, "Mimi niko ambaye niko3:14 au Nitakuwa kama Nitakavyokuwa; au, Mimi Ndiye. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: ‘Mimi niko amenituma kwenu.’ "
15 Vilevile Mungu akamwambia Musa, "Waambie Waisraeli, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amenituma kwenu.’
"Hili ndilo Jina langu milele,
Jina ambalo mtanikumbuka kwalo
kizazi hadi kizazi.