Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 3:14,15

SRUV Swahili Revised Union Version

14 Ufu 1:4,8;Kut 6:3;Yn 8:58;Ebr 13:8Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;3:14 Au, Nitakuwa kama Nitakavyokuwa; au, Ndimi Ndiye. akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO3:14 Au, Nitakuwa; au, Ndimi. amenituma kwenu.

15 Zab 135:13;Hos 12:5Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, BWANA,3:15 Neno hili BWANA au MUNGU lionekanapo kuandikwa kwa herufi kubwa, laonesha jina takatifu sana la Mwenyezi Mungu. Katika Kiebrania huwa YHWH (latamkwa Yahweh). Katika Lugha ya Kiebrania neno YHWH laasilika kwa kiarifa ‘hayah’ ambalo tafsiri yake ni ‘kuwa’ Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    14 Mungu akamwambia Musa, "Mimi niko ambaye niko3:14 au Nitakuwa kama Nitakavyokuwa; au, Mimi Ndiye. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: ‘Mimi niko amenituma kwenu.’ "

    15 Vilevile Mungu akamwambia Musa, "Waambie Waisraeli, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amenituma kwenu.’

    "Hili ndilo Jina langu milele,

    Jina ambalo mtanikumbuka kwalo

    kizazi hadi kizazi.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    14 Mungu akamwambia Mose, "Mimi niko ambaye niko. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: ‘Mimi niko amenituma kwenu.’ "

    15 Vilevile Mungu akamwambia Mose, "Waambie Waisraeli, ‘Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo amenituma kwenu.’ Hili ndilo Jina langu milele, Jina ambalo mtanikumbuka kwalo kutoka kizazi hadi kizazi.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.