Musa na utukufu wa Mwenyezi Mungu
12 Musa akamwambia Mwenyezi Mungu, "Umekuwa ukiniambia, ‘Ongoza watu hawa,’ lakini hujanifahamisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Umesema, ‘Ninakujua wewe kwa jina lako, nawe umepata kibali mbele zangu.’ 13 Ikiwa umependezwa nami, nifundishe njia zako ili nipate kukujua, nami nizidi kupata kibali mbele zako. Kumbuka kuwa taifa hili ni watu wako."
14 Mwenyezi Mungu akajibu, "Uso wangu utaenda pamoja nawe, nami nitakupa raha."
15 Kisha Musa akamwambia, "Kama Uso wako hauendi pamoja nasi, usituondoe hapa. 16 Mtu yeyote atajuaje kuwa mimi pamoja na watu wako tumepata kibali mbele zako, usipoenda pamoja nasi? Ni nini kingine kitakachoweza kututofautisha mimi na watu wako miongoni mwa watu wengine wote walio katika uso wa dunia?"
17 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, "Nitakufanyia jambo lile uliloomba, kwa sababu ninapendezwa nawe, nami ninakujua kwa jina lako."