Maombezi ya Musa kwa Mungu
12 Zab 1:6;Yer 1:5;Yn 10:14;2 Tim 2:19Musa akamwambia BWANA, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Lakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu. 13 Kut 34:9;Zab 25:4;27:11;Kum 9:26;Yoe 2:17Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unioneshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. 14 Kut 40:34-38;Isa 63:9;Kum 3:20;Yos 21:44;22:4;23:1;Zab 95:11Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. 15 Kut 34:9Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. 16 Hes 14:14;Kum 4:34;2 Sam 7:23;Zab 147:20;Tit 2:14Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi? 17 Mwa 19:21;Yak 5:16BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako.