3 Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, 4 "Kwangu mimi, hili ndilo agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. 5 Hutaitwa tena Abramu17:5 maana yake Baba aliyetukuka, bali jina lako litakuwa Ibrahimu17:5 maana yake Baba wa wengi, kwa maana nimekufanya baba wa mataifa mengi. 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana; kwako yatatoka mataifa, na wafalme watatoka kwako. 7 Nitalithibitisha agano langu kama agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo, nami nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazao wako. 8 Nchi yote ya Kanaani, unayoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na ya uzao wako; nami nitakuwa Mungu wao."
9 Ndipo Mungu akamwambia Ibrahimu, "Kwako wewe, lazima ushike agano langu, wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo. 10 Hili ni agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa. 11 Mtatahiriwa, na hii itakuwa ni alama ya agano kati yangu na ninyi.