Onyo dhidi ya kutokuamini
7 Kwa hiyo, kama Roho wa Mungu asemavyo:
"Leo, mkiisikia sauti yake,
8 msiifanye mioyo yenu migumu,
kama mlivyofanya katika uasi,
wakati ule wa kujaribiwa jangwani,
12 Ndugu zangu, chungeni asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu aliye hai. 13 Lakini mtiane moyo mtu na mwenzake kila siku, maadamu inaitwa "Leo", ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 15 Kama ilivyonenwa:
"Leo, mkiisikia sauti yake,
msiifanye mioyo yenu migumu
kama mlivyofanya wakati wa kuasi."