Pular para o conteúdo
Publicidade

Jó 25

Bildadi anasema: Mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mwenyezi Mungu?

1 Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu:

2 "Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu;

yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.

3 Je, majeshi yake yaweza kuhesabika?

Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?

4 Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?

Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?

5 Ikiwa hata mwezi sio mwangavu

nazo nyota si safi machoni pake,

6 sembuse mtu ambaye ni funza:

mwanadamu ambaye ni buu tu!"

Veja também