5 Mabaharia wote waliogopa na kila mmoja akamlilia mungu wake mwenyewe. Nao wakatupa mizigo baharini ili meli ipungue uzito.
Lakini Yona alikuwa ameteremkia chumba cha ndani ya meli, ambapo alilala na kupatwa na usingizi mzito. 6 Nahodha akamwendea na kusema, "Wewe unawezaje kulala? Amka ukamwite mungu wako! Huenda akatuangalia, tusiangamie."