5 Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hadi pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi. 6 Zab 78:34;Mt 8:25Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee.
Yona 1:5,6
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
5 Mabaharia wote waliogopa na kila mmoja akamlilia mungu wake mwenyewe. Nao wakatupa mizigo baharini ili meli ipungue uzito.
Lakini Yona alikuwa ameteremkia chumba cha ndani ya meli, ambapo alilala na kupatwa na usingizi mzito. 6 Nahodha akamwendea na kusema, "Wewe unawezaje kulala? Amka ukamwite mungu wako! Huenda akatuangalia, tusiangamie."
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
5 Mabaharia wote waliogopa na kila mmoja akamlilia mungu wake mwenyewe. Nao wakatupa mizigo baharini ili meli ipungue uzito.
Lakini Yona alikuwa ameteremkia chumba cha ndani ya meli, mahali ambapo alilala na kupatwa na usingizi mzito. 6 Nahodha akamwendea na kusema, "Wewe unawezaje kulala? Amka ukamwite mungu wako! Huenda akatuangalia, tusiangamie."
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.