Neno alifanyika mwili
1 Hapo mwanzo alikuwako Neno, naye huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
14 Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba1:14 Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu., amejaa neema na kweli.