21 Martha akamwambia Isa, "Bwana, kama ungekuwa hapa, ndugu yangu hangekufa. 22 Lakini sasa ninajua kuwa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa."
23 Isa akamwambia, "Ndugu yako atafufuka."
24 Martha akamjibu, "Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho."
25 Isa akamwambia, "Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi; 26 na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?"
27 Martha akamwambia, "Ndiyo Bwana, ninaamini ya kuwa wewe ndiwe Al-Masihi11:27 Al-Masihi maana yake Aliyetiwa mafuta., Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni."