6 Nami nikasema, "Aa, Bwana Mungu Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu."
7 Lakini Mwenyezi Mungu akaniambia, "Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza. 8 Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe," asema Mwenyezi Mungu.