4 Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, awaambialo wale wote niliowapeleka kutoka Yerusalemu kwenda uhamishoni Babeli: 5 "Jengeni nyumba na mwishi humo, pandeni bustani na mle mazao yake. 6 Oeni wake na mzae watoto wa kiume na wa kike; watafutieni wake watoto wenu wa kiume, na waozeni binti zenu ili nao wazae watoto wa kiume na wa kike; mkaongezeke huko, wala msipungue idadi. 7 Pia tafuteni amani na mafanikio ya mji ambamo nimewapeleka uhamishoni. Mwombeni Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mji huo, kwa sababu ukistawi, ninyi pia mtastawi."
10 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: "Miaka sabini itakapotimia kwa ajili ya Babeli, nitakuja kwenu na kutimiza ahadi yangu ya rehema ya kuwarudisha mahali hapa. 11 Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Mwenyezi Mungu, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.