Publicidade

Jeremias 31

31 "Siku zinakuja," asema Mwenyezi Mungu,

"nitakapofanya agano jipya

na nyumba ya Israeli

na nyumba ya Yuda.

32 Halitafanana na agano

nililofanya na baba zao

wakati nilipowashika mkono

kuwaongoza watoke Misri,

kwa sababu walivunja agano langu,

ijapokuwa nilikuwa mume kwao,"

asema Mwenyezi Mungu.

33 "Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli

baada ya siku zile," asema Mwenyezi Mungu.

"Nitaweka sheria yangu katika nia zao,

na kuiandika mioyoni mwao.

Nitakuwa Mungu wao,

nao watakuwa watu wangu.

34 Mtu hatamfundisha tena jirani yake,

wala mtu kumfundisha ndugu yake, akisema,

Mjue Mwenyezi Mungu,

kwa sababu wote watanijua mimi,

kuanzia aliye mdogo hata aliye mkubwa kuliko wote,"

asema Mwenyezi Mungu.

"Nitasamehe uovu wao, wala sitazikumbuka dhambi zao tena."

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-