20 Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akasujudu na kuabudu, 21 akasema:
"Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi,
nami nitaondoka uchi1:21 au nitarudi huko uchi,
Mwenyezi Mungu alinipa,
naye Mwenyezi Mungu ameviondoa;
jina la Mwenyezi Mungu litukuzwe."