Mwenyezi Mungu amjibu Ayubu
1 Kisha Mwenyezi Mungu akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema:
2 "Nani huyu atiaye mashauri yangu giza
kwa maneno yasiyo na maarifa?
3 Jikaze kama mwanaume;
nitakuuliza swali,
nawe unijibu.
4 "Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia?
Niambie, kama unafahamu.