Pular para o conteúdo
Publicidade

Ayubu 38

4 "Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia?

Niambie, kama unafahamu.

5 Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake?

Hakika wewe unajua!

Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake?

6 Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini,

au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni,

7 wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,

na malaika wote walipokuwa wakishangilia kwa furaha?

8 "Ni nani aliyeifungia bahari milango

ilipopasuka kutoka tumbo,

9 nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake,

na kuyafungia katika giza nene,

10 nilipoamuru mipaka yake,

na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,

11 niliposema, Unaweza kufika hapa, wala si zaidi;

hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea?

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também