Isa nyumbani mwa Farisayo
1 Siku moja ya Sabato, Isa alipoenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo, watu walikuwa wakimchunguza kwa makini. 2 Hapo mbele yake palikuwa na mtu mmoja mwenye ugonjwa wa kuvimba mwili. 3 Isa akawauliza wale Mafarisayo na walimu wa Torati, "Je, ni halali kuponya watu siku ya Sabato au la?" 4 Wakakaa kimya. Hivyo Isa akamshika yule mgonjwa mkono na kumponya, akamruhusu aende zake.