Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 8

Isa atuliza dhoruba

22 Siku moja Isa alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, "Tuvukeni hadi ng’ambo ya ziwa." Nao wakaondoka. 23 Hivyo walipokuwa wakienda, akalala usingizi. Dhoruba kali ikatokea mle ziwani, hata mashua ikawa inajaa maji, nao walikuwa katika hatari kubwa.

24 Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, "Bwana8:24 Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita "Bwana" kwa heshima ya kawaida., Bwana, tunaangamia!"

Yeye akaamka, akaukemea ule upepo na yale mawimbi; dhoruba ikakoma, nako kukawa shwari. 25 Akawauliza wanafunzi wake, "Imani yenu iko wapi?"

Kwa woga na mshangao wakaulizana, "Huyu ni nani, ambaye anaamuru hata upepo na maji, navyo vikamtii?"

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também