Pular para o conteúdo
Publicidade

Marcos 11

Mtini ulionyauka

20 Kesho yake asubuhi walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umenyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake. 21 Petro akakumbuka na kumwambia Isa, "Mwalimu, tazama! Ule mtini ulioulaani umenyauka!"

22 Isa akawajibu, "Mwaminini Mungu. 23 Amin, nawaambia, mtu yeyote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini,wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, atatimiziwa. 24 Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu. 25 Nanyi kila msimamapo kusali, sameheni mkiwa na neno na mtu, ili naye Baba11:25 Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi. yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu. [

Veja também