Njama ya kumuua Isa
1 Zilikuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka14:1 Sherehe iliyowakumbusha Waisraeli jinsi Mwenyezi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani huko Misri., na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walikuwa wakitafuta njia ya kumkamata Isa kwa hila na kumuua. 2 Lakini walisema, "Tusilifanye jambo hili wakati wa Sikukuu, maana watu wanaweza wakafanya ghasia."
Isa apakwa mafuta huko Bethania
(Mathayo 26:6-13; Luka 7:35-38; Yohana 12:1-8)