Pular para o conteúdo
Publicidade

Marcos 4

37 Kukawa na dhoruba kali, nayo mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikawa karibu kujaa maji. 38 Isa alikuwa katika shetri, akiwa analala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, "Mwalimu, hujali kama tunazama?"

39 Akaamka, akaukemea ule upepo, akayaambia yale mawimbi, "Uwe kimya! Tulia!" Ule upepo ukatulia, kukawa shwari kabisa.

40 Isa akawaambia wanafunzi wake, "Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?"

41 Nao wakawa wameogopa sana, wakaulizana, "Ni nani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!"

Veja também