14 Mfalme Herode akasikia habari hizi, kwa maana jina la Isa lilikuwa limejulikana sana. Watu wengine walikuwa wakisema, "Yahya amefufuliwa kutoka kwa wafu, ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake."
15 Wengine wakasema, "Yeye ni Ilya."
Nao wengine wakasema, "Yeye ni nabii, kama mmoja wa manabii wa zamani."
16 Lakini Herode aliposikia habari hizi, akasema, "Huyo ni Yahya, niliyemkata kichwa, amefufuliwa kutoka kwa wafu!"