Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 1

Kumbukumbu za ukoo wa Isa Al-Masihi

1 Habari za ukoo wa Isa Al-Masihi mwana wa Daudi1:1 Mariamu, mamake Isa, na pia Yusufu, baba mlezi wa Isa, walitokea ukoo wa Mfalme Daudi. Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (Zaburi 89:3-4)., mwana wa Ibrahimu:

2 Ibrahimu akamzaa Isaka,

Isaka akamzaa Yakobo,

Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake,

3 Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari,

Peresi akamzaa Esromu,

Esromu akamzaa Aramu,

4 Aramu akamzaa Aminadabu,

Aminadabu akamzaa Nashoni,

Nashoni akamzaa Salmoni,

5 Salmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu,

Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu,

Obedi akamzaa Yese,

6 Yese akamzaa Daudi, aliyekuwa mfalme.

Daudi akamzaa Sulemani, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.

7 Sulemani akamzaa Rehoboamu,

Rehoboamu akamzaa Abiya,

Abiya akamzaa Asa,

8 Asa akamzaa Yehoshafati,

Yehoshafati akamzaa Yoramu,

Yoramu akamzaa Uzia,

9 Uzia akamzaa Yothamu,

Yothamu akamzaa Ahazi,

Ahazi akamzaa Hezekia,

10 Hezekia akamzaa Manase,

Manase akamzaa Amoni,

Amoni akamzaa Yosia,

11 wakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.

12 Baada ya uhamisho wa Babeli:

Yekonia alimzaa Shealtieli,

Shealtieli akamzaa Zerubabeli,

13 Zerubabeli akamzaa Abihudi,

Abihudi akamzaa Eliakimu,

Eliakimu akamzaa Azori,

14 Azori akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Akimu,

Akimu akamzaa Eliudi,

15 Eliudi akamzaa Eleazari,

Eleazari akamzaa Matani,

Matani akamzaa Yakobo,

16 naye Yakobo akamzaa Yusufu, aliyekuwa mumewe Mariamu, mama yake Isa, aitwaye Al-Masihi.1:16 Al-Masihi maana yake Aliyetiwa mafuta.

17 Hivyo, kulikuwa na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Ibrahimu hadi Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho wa Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho wa Babeli hadi Al-Masihi.

Veja também