Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 12

Ishara ya Yona

38 Kisha baadhi ya Mafarisayo na walimu wa Torati wakamwambia, "Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako."

39 Lakini yeye akawajibu, "Kizazi kiovu na cha uzinzi kinaomba ishara! Lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya nabii Yona. 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la samaki mkubwa sana kwa siku tatu, usiku na mchana, vivyo hivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika moyo wa nchi siku tatu, usiku na mchana.

Veja também