Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 20

Isa awaponya vipofu wawili

29 Isa na wanafunzi wake walipokuwa wakiondoka Yeriko, umati mkubwa wa watu wakamfuata. 30 Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Isa alikuwa anapita, wakapaza sauti wakisema, "Bwana Isa, Mwana wa Daudi20:30 Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (Zaburi 89:3-4)., tuhurumie!"

31 Umati wa watu wakawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao wakazidi kupaza sauti wakisema, "Bwana Isa, Mwana wa Daudi, tuhurumie."

32 Isa akasimama na kuwaita, akawauliza, "Mnataka niwafanyie nini?"

33 Wakamjibu, "Bwana, tunataka kuona."

34 Isa akawahurumia na kuwagusa macho yao. Mara macho yao yakapata kuona, nao wakamfuata.

Veja também