Yuda ajinyonga
3 Yuda, aliyemsaliti Isa, alipoona kuwa Isa amehukumiwa, akajuta na akarudisha vile vipande thelathini vya fedha alivyopewa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. 4 Akasema, "Nimetenda dhambi, kwa maana nimeisaliti damu isiyo na hatia."
Wakamjibu, "Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako."
5 Basi Yuda akavitupa vile vipande vya fedha ndani ya Hekalu akaondoka akaenda kujinyonga.