Isa ajaribiwa nyikani
1 Kisha Isa akaongozwa na Roho Mtakatifu wa Mungu hadi nyikani ili ajaribiwe na ibilisi. 2 Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa. 3 Mjaribu akamjia na kumwambia, "Ikiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu4:3 Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (Yohana 1:1), wa kiroho, bali si wa kimwili., amuru mawe haya yawe mikate."
4 Lakini Isa akajibu, "Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ "
7 Isa akamjibu, "Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Mwenyezi Mungu, Mungu wako.’ "
10 Isa akamwambia, "Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’ "