Wanafunzi wa kwanza wa Isa
18 Isa alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa walikuwa wavuvi. 19 Isa akawaambia, "Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu."