27 Wakampa Musa taarifa hii: "Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake. 28 Lakini watu wanaoishi huko ni wenye nguvu, na miji yao ina ngome na ni mikubwa sana. Huko tuliona hata wazao wa Anaki.
30 Kisha Kalebu akawanyamazisha watu mbele ya Musa na kusema, "Imetupasa kupanda na kuimiliki nchi, kwa maana hakika tunaweza kufanya hivyo."
31 Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, "Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kuliko sisi." 32 Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, "Nchi tuliyoipeleleza hula watu wanaoishi ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu. 33 Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili). Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona."